Mtaala wa Biblia wa Mazingira Halisia (MBMH)
Mbinu ya Mtaala wa Biblia wa Mazingira Halisia (MBMH) unafanana na aina nyingine za mtaala wa Biblia zinazohusisha wataalamu wa Biblia wanaojihusisha na jamii, wanataalumu watakao mageuzi katika jamii, na ‘wasomaji’ wa Biblia Wakristo wa Kawaida (wanaojua kusoma au la).
Wengi mnaifahamu mbinu ya Tazama-Amua-Tenda, ambayo mtaala wa Biblia unaanza na uchambuzi yakinifu wa mazingira halisia ya jamii (Tazama), kisha Biblia inasomwa tena ili kuhusianisha maandiko ya Biblia na mazingira ya maisha halisia (Amua), na kisha tunaendelea kwenye hatua ya kutenda pale tunapoitikia kile ambacho Mungu anasema (Tenda). Uchambuzi yakinifu wa mazingira halisia ya jamii hutuwezesha kuelewa maisha yetu halisia; kuisoma Biblia tena na tena hutuwezesha kuamua ikiwa maisha yetu halisia yako vile Mungu anavyotazamia yawe; mpango wetu wa utekelezaji hutuwezesha kutenda kazi na Mungu ili kubadili hali halisi ya maisha yetu. Mchakato huu ni endelevu, kwa kuwa kila tendo moja hutuongoza katika hatua ya kutafakari (Tazama), nk. Hili ni duara la theologia ya vitendo, yaani kutafakari na kutenda na kisha kutafakari tena yale tuliyotenda, yaani kutafakari-kutenda-kutafakari tena.