SHUGHULI ZA UJAMAA

Kila idara ndani ya Kituo cha Ujamaa ina muundo na mipango yake ambayo inajibu mahitaji muhimu ya maisha halisia. Tangu tulipoanza mwaka 1989, tumejitahidi kushughulikia mahitaji ya maisha halisia ya jamii. Kila idara inajihusisha na mambo maalumu yaliyopo katika uchambuzi wetu wa kijamii na kitheologia; hata hivyo, idara zetu zote zinafanyakazi pamoja, zinamshikamano na zina uwiano katika mambo mengi.

Kila Idara inafuata Lengo Kuu la Kituo cha Ujamaa:

* Lengo letu kuu ni kuwahamasisha, kuwafundisha, kuwawezesha na kuwatia nguvu maskini, tabaka la wafanyakazi, na wanyonge. Tunafanya kazi hususani na wanawake, vijana, watu waishio na VVU/UKIMWI, na watu wasio na ajira. Tunafanya kazi hii kwa ajili ya makusudi ya ufalme wa Mungu na kwa ajili ya jamii kuwa na uzima tele kwa watu wote (Yohana 10:10).

* Pale ambapo makusudi yetu yanapatana na jamuiya za kidini, serikali, na jumuiya za kijamii, tunashirikiana pamoja kwa ajili ya mabadiliko ya jamii.

* Raslimali na zana zetu za msingi kwa kazi hii ni za kibiblia na kitheologia, sambamba na kutumia Mtaala wa Biblia wa Mazingira Halisia, na mbinu ya Tazama, Amua na Tenda. Kila inapowezekana, tunatumia lugha za wenyeji tunaoshirikiana nao katika jamii husika.

* Mkazo wetu uko katika kanuni ya kutafakari na kutenda, yaani dhana ya theologia ya vitendo.

Lengo hili kuu limepewa nafasi yake katika kila Idara yetu. Licha ya Idara tajwa, Kituo cha Ujamaa huendesha mihadhara ya kila mwaka na Kampeni maalumu, kama vile Kampeni ya Tamari na Kampeni ya Jumapili ya Wafanyakazi.



Contact Webmaster | View the Promotion of Access to Information Act | View our Privacy Policy
© University of KwaZulu-Natal: All Rights Reserved