MUUNDO WA KITUO CHA UJAMAA

Kampeni ya Tamari

Mpango huu wa kampeni ya Tamari ulianzishwa ili kushughulikia maswala mbalimbali yanayogusa wanawake na jinsia; hakika kampeni hii ni shughuli muhimu katika idara zetu za ujamaa. Hasa kampeni hii inashughulika na wanawake na wasichana ambao ni wahanga wa ukatili wa kijinsia. Kampeni hii pia inashughulikia maswala ya wanaume, kwa kuweka wazi ukweli kwamba wanaume wamehusika na ukatili wa kijinsia. zaidi, kampeni hii inagusa makanisa moja kwa moja, ili kuyafanya yawe mahali salama kwa ajili ya kuzungumzia ukatili wa kijinsia na maswala ya jinsia kwa ujumla.

Kampeni hii pia inashughulika moja kwa moja na uhusiano uliyopo kati ya jinsia na VVU/UKIMWI na utawala (maswala ambayo Kituo cha Ujamaa kina umahiri mkubwa). Habari ya Tamari haihusiani na ukatili wa kijinsia tu, pia ni habari inayohusu jinsi familia na serikali vilivyoshindwa kuwalinda wanawake, na kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia katika nyanja nyingine za maisha. Kampeni hii husaidia kuweka bayana maswala mbalimbali ya kijinsia.

Kitu cha pekee katika mpango huu wa kampeni ni kwamba unaweza kutumika katika mazingira karibu yote ya maisha. Mpango huu wa Kampeni ya Tamari umeshatumika mahali mbalimbali katika mazingira ya bara letu la Afrika. Kama watu wanaweza kupata mafunzo na zana muafaka basi Kampeni ya Tamari inaweza kuwa na mguso wa pekee katika bara letu.


Kampeni ya Jumapili ya Mfanyakazi

Mpango huu ni wa kampeni maalumu kwa ajili ya mafundisho ya kibiblia yahusuyo haki kwa wafanyakazi Wakristo, kwa kusisitiza haki yao ya kufanya kazi na kupumzika. Kampeni hii hufanya suala la kazi na mambo mengine yahusuyo kazi yawe wazi katika kanisa. Kampeni hii pia hutumika kuliwezesha kanisa kushughulikia tatizo la ukosefu wa ajira kwa waumini wake. Kampeni hii hufanyika Jumapili katika wiki la Mei Mosi, na hufanywa na wafanyakazi Wakristo na watumishi wa Kanisa ili kumtafakari Mungu aliye mtendakazi mkuu.

JUMAPILI YA MFANYAKAZI NI NINI?

Kipindi cha Ubaguzi wa Rangi, wakati tabaka la wafanyakazi weusi walipokandamizwa kiukatili, wakadharirishwa utu wao na kunyanyaswa, kanisa liliamua kuwaunga mkono waliodharauliwa na kupuuzwa katika jamii – yaani tabaka la wafanyakazi.

Changamoto kuu iliyolikabili kanisa wakati huo ilikuwa namna gani linaweza kufundisha kwa wazi mafundisho yake kuhusu jamii; kanisa liliweza kufundisha kuhusu haki maeneo ya kazi kwa kupitia Kampeni ya Jumapili ya Mfanyakazi iliyohamasisha madhehebu mbalimbali katika ibada zao kuonyesha mshikamano na watu wasio na ajira. Mkazo katika ibada ulikuwa juu ya ujumbe wa Biblia kuhusu haki, na ya kwamba Biblia inatufundisha kuwa Mungu ni Mfanyakazi. Ikiwa sehemu ya mchakato wa kampeni, vipeperushi vilisambazwa kwa watu na matangazo yalibandikwa katika makanisa yote. Mifano ya mahubiri, vifungu vya maandiko na nyimbo zenye mlengo wa mageuzi ya jamii vilitumwa kwa wachungaji, mapadre, na mashirika ya Kikristo yanayojihusisha na masuala ya haki ya kiuchumi na jamii. Haya yote yalifanyika kwa maandalizi ya ibada za Kampeni ya Jumapili ya Mfanyakazi.

Tangu mwaka 1979, ujumbe wa Jumapili ya Mfanyakazi umelenga zaidi mazingira ya kazi na haki za mfanyakazi; mlengo huu ulibadilika kuanzia mwaka 1994 kutokana na Katiba Mpya na Sheria za Kazi zinazomlinda mfanyakazi asikandamizwe. Hata hivyo, katika miaka 21 ya demokrasia, Sheria za Kazi zinaonekana kupuuzwa na Wamiliki wa Njia za Uzalishaji, kama ilivyotokea katika Mauaji ya Marikana, Afrika Kusini, tarehe 16 Agosti 2012, wakati wakuu wa

mgodi uitwao LonMin walipokataa ombi la wafanyakazi la nyongeza ya mshahara baada ya mgomo wa muda mrefu zaidi katika historia ya Afrika Kusini.

Hawa walikuwa ni wafanyakazi maskini zaidi katika sekta ya uchimbaji wa madini wakihangaikia kipato cha kuwawezesha kuishi tu katikati ya utajiri mkubwa wa mabepari wakuu wa kampuni ya madini ya LonMin. Hili ni suala la haki ya kiuchumi. Kampeni ya Jumapili ya Mfanyakazi ni harakati ya kupaza sauti kwamba Kanisa liunge mkono Mapambano ya Wafanyakazi kwa ajili ya ‘Mshahara Unaotosha Kuishi’.


CEBI (ni kutuo cha mtaala ya Biblia kama yetu, kiko Brazil) kinatupa faida ya mambo mawili katika mchakato wa duara la theoloiga ya vitendo. Mchakato wao una vipengere vya Tazama-Amua-Tenda-Sherekea-Tathmini. Baada ya kutenda, kundi husherekea kile walichofaulu kufanya katika jamii, hufanya hivyo kiliturgia na kijamii. Na baada ya sherehe hufuata tathmini. Kundi hutathmini mchakato mpaka walipofikia, na kisha huendelea kuweka mpango wa kazi inayoendelea.

Mtaala wa Biblia wa Mazingira Halisia ni mojawapo ya mfumo wa kanuni ya Tazama-Amua-Tenda. Kwanza, Mtaala wa Biblia wa Mazingira Halisia huzingatia uchambuzi yakinifu na mahitaji ya jamii husika ya maskini, tabaka la wafanyakazi, na wanyonge. Mtazamo wao wa maisha halisia ndiyo msingi wa mtaala wote wa Biblia. Pili, Mtaala wa Biblia wa Mazingira Halisia unatoa fursa ya kufanya uchambuzi yakinifu wa kitheologia, kutuwezesha “kusoma ishara za nyakati”. Biblia husomwa kwa uangalifu na kwa ukaribu sana ili kusikia sauti maalumu katika maandiko ya Biblia na katika mazingira yake ya kihistoria na kijamii, na kutuwezesha kupata zana za kitheologia za kutuwezesha kutafakari na kufanya uchambuzi yakinifu wa jamii. Na tatu, Mtaala wa Biblia wa Mazingira Halisia huhitimishwa kwa kutumia zana na raslimali za kitheologia kwa ajili ya kupanga mabadiliko ya mtu binafsi na ya jamii.Contact Webmaster | View the Promotion of Access to Information Act | View our Privacy Policy
© University of KwaZulu-Natal: All Rights Reserved